Milipuko mikubwa yatokea mjini Mogadishu
Milipuko miwili mikubwa imetokea katikati mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Walioshuhudia tukio hilo wamesema.
Kwa mujibu wa afisa wa polisi Meja Mohamed Hussein mlipuko wa kwanza umetokea karibu na wizara ya kazi eneo ambalo zipo wizara nyingine vile vile ambapo bomu lililotegwa ndani ya gari lililipuka.
Amesema mashambulizi hayo ni ya kujitoa muhanga. Hata hivyo, polisi nchini Somalia hawajatoa taarifa zaidi.
Kundi la kigidi la al-Shabab mara nyingi huwa linahusika na mashambulizi ya mabomu yanayoyalenga maeneo ya umma na ofisi za serikali.
Kundi hilo la al-Shabaab linataka kuiondoa serikali iliyopo madarakani inayoungwa mkono na nchi za magharibi.
No comments