Ripoti ya Urusi kujiingiza kwenye uchaguzi wa Marekani yawasilishwa
Mwanasheria maalumu nchini Marekani Robert Mueller amewasilisha ripoti iliyokuwa inasubiriwa kwa muda mrefu juu ya uchunguzi kuhusu kujiingiza kwa Urusi katika uchaguzi wa rais nchini Marekani mnamo mwaka 2016.
Rais Donald Trump ameushutumu uchunguzi huo na kusema kuwa ni njama za kumwandama. Hata hivyo, mwanasheria huyo maalumu ameukamilisha uchunguzi huo bila ya kupendekeza mashtaka mapya.
Rais Trump anayedaiwa kuzuia mkondo wa sheria na kushirikiana na Urusi, anaweza kuhusishwa na makosa mazito yanayoweza kusababisha aondolewe madarakani kwa njia za kisheria.
Muda mfupi baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa wabunge wa chama cha upinzani cha Democratic wametoa wito kwamba ripoti hiyo itolewe kikamilifu, ikiwa ni pamoja na ushahidi wa msingi la sivyo wametishia kufungua mashtaka mahakamani.
No comments