Shomari Kapombe mbioni kurejea Simba SC
Beki wa Simba, Shomari Kapombe sasa yuko vizuri na anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi wiki ijayo.
Kapombe amesema amefanyiwa vipimo na wamebaini kwa sasa yupo vizuri na ameanza mazoezi mepesi.
“Nilienda Afrika Kusini kufanyiwa vipimo ili kujua maendeleo yangu yako vipi, kwa sasa vipimo vinaonyesha nipo vizuri na nimerejea nchini na sasa kuwa mazuri nitaungana na timu kuanza mazoezi lakini kwa sasa namshukuru Mungu niko fiti kiafya,” alisema Kapombe.
Kapombe aliumia kifundo cha mguu kwenye kambi ya Taifa Stars iliyowekwa nchini Afrika Kusini ambako walikuwa wakijiandaa na mechi dhidi ya Lesotho, beki huyo alifanyiwa upasuaji.
No comments