Naibu Waziri auliwa na Al Shabaab Somalia
Wanamgambo wa Al-Shabaab wavamia jengo la Serikali Jijini Mogadishu na kuua watu takribani 11 akiwemo naibu waziri wa ajira. Shambulio hilo la risasi lilitokea muda mfupi baada ya shambulio la kujitoa mhanga kwenye gari lililotokea karibu na jengo hilo.
Al-Shabaab wamekiri kuhusika na shambulio hilo lililojeruhi wengine takribani 10, shambulio hilo limetokea karibu sana na Makao Makuu ya Intelijensia ya nchi hiyo.
Shambulio kama hili lilifanyika mwishoni mwa Februari na kuua takribani watu 24 ambapo kabla ya hapo kulikuwa na milipuko miwili ya kujitoa mhanga.
Al Shabaab ndicho kikundi hai zaidi cha wanamgambo wenye lengo la kuitoa Serikali ya Somalia inayopewa nguvu na mataifa ya Magharibi.
No comments