Breaking News

Upanuzi na uboreshaji wa barabara za mitaa imeharibu miundombinu ya maji Bukoba


Na, Clavery Christian; Bukoba. 

Mamlaka ya maji wilayani Bukoba mkoani Kagera imesema kuwa upanuzi na uboreshaji wa barabara za mitaa umechangia kuharibika kwa baadhi ya miundombinu ya maji na kupelekea baadhi ya maeneo kukosa huduma ya maji kwa wakati. 

Hayo yamesemwa na Bi, Rosada Antelmy Afisa Utumishi ambaye ni kaimu wa afisa uhusiano wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira BUWASA wakati akiongea na muungwana blog ofisini kwake katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji hapa nchini. 

 Bi Rosada Antelmy amesema kuwa wao kama mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira wameamua kutembelea wateja wao wote na kuongea nao na kuwarejeshea huduma ya maji wale waliokatiwa kutokana na kulimbikiza madeni huku wakitembelea vyanzo vya maji na kufanya usafi katika vyanzo vya maji. 

Bi, Rosada amewataka wananchi kutoa taarifa pale wanapoona miundo mbinu ya maji imeharibiwa katika mamlaka husika ili waweze kuikarabati na wateja waendelee kupata huduma ya maji. 

Aidha amesema kuwa wameongeza wateja wapya katika mitaa mipya ambapo wanaendelea na zoezi la kuwaunganishia huduma ya maji.

No comments