ULITAKA KUFAHAMU KAULI YA MBOWE BAADA YA KUPEWA DHAMANA? SOMA HAPA
Saa chache baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kumuachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko, viongozi hao wameshindwa kuzungumza chochote.
Akizungumza Jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu (CHADEMA) Zanzibar Salum Mwalimu amesema kwa sasa viongozi hao hawawezi kuzungumza chochote baada ya kukaa rumande kwa miezi mitatu hivyo wanachofanya sasa ni kupatiwa maelezo kuhusu muenendo wa chama hicho.
"Hukumu ni hukumu ingawaje tulijua tutashinda, lakini tunamshukuru Mungu kwa kilichotokea, itakuwa jambo la ajabu sana kusema Mwenyekiti na Matiko walikuwa wamejipanga kuongea."amesema Mwalimu
"Miezi mitatu si midogo, ukitoka muda huu kichwa kinakuwa kinataka kila jambo, kwa hiyo naomba tuwape muda kidogo na mwishoni mwa wiki hii tutazungumza na waandishi wa habari." ameongoza Mwalimu
Mbowe na Matiko walikataa rumande kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya kunyimwa dhamana na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba , 2018.
No comments