Samatta asepa Ubelgiji 'Mpaka wakati ujao, asanteni sana'
Baada ya usiku wa jana, kushuhudiwa historia kubwa katika Uwanja wa Taifa ambapo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefuzu michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON baada ya miaka 39.
Hiyo ni baada ya kuifunga timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes" kwa mabao 3-0, mabao yaliyofungwa na Simon Msuva, Erasto Nyoni na Aggrey Morris.
Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ni miongoni mwa wachezaji waliocheza kwa kiwango cha juu katika mchezo huo, mara baada ya kumalizika kwa mchezo alikwea pipa na kurejea Ubelgiji katika klabu yake ya Genk.
Pia wakati anaondoka katika Uwanja wa Ndege wa JNIA kuelekea Ubelgiji, majira ya saa 7 za usiku, Samatta aaliandika ujumbe, "mpaka wakati ujao, ahsanteni sana", ukionesha kuwa yuko safarini kurejea klabuni kwake.
Taifa Stars imeungana na timu ya taifa ya Uganda, Kenya na Burundi zitakazoiwakilisha Afrika Mashariki katika michuano ya AFCON itakayofanyika kuanzia mwezi June hadi Julai, 2019 nchini Misri.
No comments