Breaking News

Rais Magufuli afanya mabadiliko madogo Baraza la Mawaziri



Taarifa rasmi kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ambayo imetolewa leo Machi 03 ni kuwa Rais Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. 

Rais Magufuli amemteua Dk. Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na pia amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Mawaziri hao wanatarajia kuapishwa Ikulu kesho tarehe 04 Machi 2019 saa 3:30 asubuhi, Taarifa rasmi ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ni kama inavyoonekana hapo chini. 

No comments