Breaking News

Profesa amwagiwa sifa baada ya kumbeba mtoto wa mwanafunzi wake



Katika hali isiyokuwa ya kawaida Profesa mmoja wa hesabu nchini Marekani amepokea sifa nyingi kutoka kwa watu tofauti tofauti mara baada ya kusambaa mitandaoni picha yake akiwa amembeba mtoto wa mwanafunzi wakati akifundisha darasani. 

Baba wa mtoto huyo Wayne Hayer aliamua kuja na mtoto wake darasani bada ya kukosa mtu wa kumsaidia kumlea mtoto huyo nyumbani. 

Mwalimu huyo aliamua kumbeba mtoto huyo kwa muda wa dakika 50 wa kipindi chake chote kwa nia ya kumpa fursa mwanafunzi wake Hayer kuandika dondoo ya kile alichokuwa anakifundisha. 

"Sijabahatika kuwa na mtoto hivyo hata wakati nambeba mtoto huyu nilikuwa nna hofu kuwa atalia, lakini cha ajabu ni kuwa alikuwa ametulia vizuri sana". 

Profesa Alexander anafundisha katika darasa la wanaume lililoko kwenye chuo cha kihistoria cha watu weusi huko Atlanta, Georgia.

No comments