Mbowe, Matiko kusuka au kunyoa leo
Mahakama Kuu Dar es Salaam leo Alhamis Machi 7, 2019 inatarajiwa kutoa hukumu kwenye maombi ya rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Esther Matiko wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi na. 112/2018 inayowakabili baadhi ya voingozi wakuu wa Chama na wabunge 7 wa CHADEMA.
Uamuzi huo wa kutoa hukumu hiuyyo leo ulitolewa jana mahakamani hapo na Jaji Rumanyika, baada ya Mahakama Kuu kusikiliza hoja za pande zote mbili katika shauri hilo, upande wa warufani (utetezi) na wajibu rufaa (Jamhuri).
Pamoja na masuala mengine, upande wa warufani uliwasilisha hoja kubwa mbili ambapo umeieleza mahakama hiyo kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kufuta dhamana ya wakata rufaa wakati walikuwepo mahakamani. Hoja nyingine ni kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kufuta dhamana prematurely, kabla ya kusema lolote kuhusu amana za wadhamini ambazo hadi sasa ziko pending.
Baada ya Mahakama Kuu kusikiliza hoja za pande zote mbili, wakata rufaa na wakatiwa rufaa, Rumanyika J aliamuru kuwa mahakama itatoa uamuzi wake siku ya leo saa saba mchana
No comments