Kocha Hans Van Der Pluijm 'akwama kusepa' Azam FC
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans Van Der Pluijm ameshindwa kuondoka nchini kwa wakati mara baada ya kufukuzwa kazi na timu hiyo.
Mratibu wa Azam FC, Philip Alando, alisema Pluijm ataondoka mara tu baada ya kupatiwa haki yake ambayo bado hajaipata.
“Kocha Hans bado yupo hapa nchini na hajaondoka ila anasubiri akishalipwa ndiyo aweze kuondoka, uongozi unafanyia kazi suala lake na wakati wowote kuanzia sasa mchakato utakamilika.
Hata hivyo amesema hawezi kuweka wazi ni kiasi gani anatakiwa kulipwa kocha huyo na kusisitiza kuwa atalipwa kulingana na mkataba wake.
Azam FC iliachana na Pluijm hivi karibuni kufuatia matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mechi zao tano ikiwemo kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba SC uwanja wa Taifa Dar es Salaam

No comments