Breaking News

Kiongozi huyu wa Chadema ajiuzulu nafasi zake na kutimkia CCM


Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Makoja kilichopo katika Kata ya Ikowa Taarafa Chilonwa wilaya ya Chamwino Bw.Samwel Kusupa, amejiuzulu nafasi zote ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi (CCM). 


Akiongea na waandishi wa habari, Bw.Kusupa  amesema kuwa ameamua kuhamia CCM kwa hiari yake kutokana na harakati zinazofanywa na Rais John Pombe Magufuli kuwatetea wanyonge na kuwaleta maendeleo ya kweli katika kila ngazi.


”Tarehe ya leo  25(jana) Machi mwaka huu nimeamua kuhama Chadema na Kujiunga na CCM kwa sababu Serikali ya awamu ya tano chini Rais Dkt.Magufuli inafanya kazi nzuri na kila mpenda maendeleo anaona hivyo sioni saababu ya kulumbana na Serikali iliyopo Madaraka kwani Upinzani hauna dira ya maendeleo kwa wananchi,”amesema Kusupa. 

Aidha amesema kuwa hakuna  Mwenyekiti wa serikali ya kijiji yoyote yule anayenunuliwa na CCM bali ameamua kurudi CCM kutokana na Serikali kufanya kazi nzuri na kuwasihi wanadodoma kuhakikisha wanaichagua CCM inayotekeleza Ilani ya Chama na wananchi kupata maendeleo. 

”Kwangu ni Uzalendo kwanza hata kama ni adui yako unapomuona anafanya mambo mema kwa jamii huwa na muunga mkono hivyo nitashirikiana na Chama changu hiki na kuwaletea maendeleo wananchi kwani Chadema nilipotea tu”amesema Bw.Kusupa 


No comments