Breaking News

Kemikali zisipodhibitiwa vizuri zinaweza kuleta madhara - Waziri wa Afya



Serikali imesema kuwa itaendelea kusimamia na kudhibiti matumizi ya kemikali ili kuhakikisha hazileti madhara kwa afya za wananchi. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu leo alipokuwa kwenye mkutano na wadau wa kemikali kujadili namna ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara ya kemikali nchini.

“Kemikali zisipodhibitiwa vizuri zinaweza kuleta madhara katika afya, mazingira pamoja na kuhatarisha usalama wa nchini, ipo haja ya kuweka mazingira mazuri ya kusimamia na kudhibiti uingizaji na matumizi ya kemikali nchini ili zisilete madhara” amesema Waziri Ummy. 

Hata hivyo takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2014 zinaonyesha vifo milioni 12.6 vilitokana na mazingira duni ya kuishi, mojawapo ya kichocheo ni athari za kemikali ambazo zimekuwa zikisababisha magonjwa na vifo. 

Waziri Ummy amesema kuwa kemikali zimekuwa na athari kubwa kwa binadamu kwa kusababisha magonjwa zaidi ya 100 huku akiyataja magonjwa ya moyo, saratani, ngozi, athari katika mifumo ya fahamu, upumaji pamoja na chakula kuathiri zaidi wananchi wengi.

No comments