Breaking News

Kamanda Sungusungu achomwa moto na watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi



Na Timothy Itembe Mara. 

Siku chache baada ya Diwani kata ya Bumera kupitia chama cha mapinduzi CCM,Deogratius Ndege kuitisha mukutano wa kuwatambua wezi wa Mifugo ambao wanawasumbua watu kwa kuwaibia Ng'ombe na kutorokea wilaya Tarime na Nchi jirani ya Kenya wezi hao wamemchomea ndani makazi  wa kijiji cha Matamankwe kata ya Susunu kwa madai kuwa anawazuia kupitisha mifogo ya wezi katika maeneo ya jirani yake. 

Akiongea wakati akiwa word ya wanaume huku akiwa anauguza majeraha ya kuunguzwa na moto mwili mzima,Ayubu Athumani 33 maarufu Mang'eng'i Mgaya alisema kuwa majambazi hao walifika nyumbani kwake majira ya saa 05 uskiku wa kuamkia Machi 10,2019 huku wakiwa na mafuta ya Peterolium kwenye Dumu la lita 20. 

"Majambazi hao takilibani watu Saba walifika Nyumbani kwangu usiku majira ya saa 05 kuamkia Machi 10 mwaka 2019 huku wakiwa na mafuta ya Peterolimu ndani ya dumu la lita 20 na kuanza kunimwagia Mwilini mwangu kisha kuwasha njiti ya kiberiti na moto kuanza kuniunguza mwili mzima huku moto huo ukiunguza  dhamani ya vitu vya ndani ambavyo dhamani yake ni zaidi ya shilingi milioni sita na laki tano"alisema Athumani. 

Athumani ambaye pia ni kamanda wa Sungusungu kata ya Susuni aliongeza kusema kuwa chanzo cha kuunguzwa na majambazi hao kwa kutumia mafuta ya Peterolium ni baada ya kuwa  anawazuia Majambazi hao kupita maeneo anayo kaa wakiwa na Ng'ombe za wizi nyakati  wanatoka kuiba mifugo hiyo. 

Kwa upande wake mganga mkuu wa Word namba Tatu na Saba ya wanaume katika hospitali ya wilaya inayomilikkiwa na halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara,Benard Makonyo alikiri kumpokea mgonjwa huyo huku akiwa na majereha ya kuunguzwa na moto mwili  mzima. 

Makonyo aliongeza kuwa matukio kama hayo yanatokea mara nyingi kwa jamii ila aliwataka wanajamii kuacha kujichukulia sheria mkonono n akujilipizia kisasi badala yake watoe taarifa kwenye vyombo husika watuhumiwa kuchukuliwa hatua zinazositahili. 

Kwa pande wa jeshi la mpolisi kupitia kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya,Henry Mwaibambe alipotafutwa hakupatikana licha ya kuwa taarifa hizo ziko polisi na pia  simu yake ja kiganjani baada ya kupigiwa iliita bila kupokelewa. 

No comments